MALI-UFARANSA-UHOLANZI-MATEKA-USALAMA-HAKI

Jeshi la Ufaransa lamuokoa mateka wa Uholanzi

Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa imetangaza kwamba Sjaak Rijke, raia wa Uholanzi aliyetekwa nyara Novemba 25 mwaka 2011 na kundi la Aqmi lenye uhusiano na Al-Qaeda, ametolewa mikononi mwa watekaji nyara Jumatatu Aprili 6 mwaka 2015 na jeshi la Ufaransa.

Sjaak Rijke, hapa picha yake ilinaswa katika video iliyorushwa na Aqmi Novemba 21 mwaka 2012. Sjaak Rijke, ametolewa mikononi mwa wanajihadi na jeshi la Ufaransa Jumatatu Aprili 6 hadi, nchini Mali.
Sjaak Rijke, hapa picha yake ilinaswa katika video iliyorushwa na Aqmi Novemba 21 mwaka 2012. Sjaak Rijke, ametolewa mikononi mwa wanajihadi na jeshi la Ufaransa Jumatatu Aprili 6 hadi, nchini Mali. AFP PHOTO/AL-JAZEERA/HO
Matangazo ya kibiashara

Wanajihadi wengi wamekamatwa Jumatatu Asubuhi waki hii, wakati wa operesheni ilioendeshwa na vikosi maalumu vya jeshi la Ufaransa kwa kumuachilia huru, Sjaak Rijke, kutoka mikononi mwa wanajihadi.

Sjaak Rijke alitekwa nyara katika mji wa Tombouctou Novemba 25 mwaka 2011 na kundi la kigaidi.

Hata hivyo katika operesheni hiyo, watu kadhaa wanoaminiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Aqmi wamekamatwa.

" Rijke amesafirishwa na kuwekwa katika usalama wa kutosha katika mji wa Tessalit. Mateka huyo yuko salama salimini", wizara ya ulinzi imesema katika tangazo ililoweka hewani katika intaneti.

Rais wa Ufaransa, François Hollande, amesema kuwa operesheni hiyo ya kumuokoa mateka wa Uholanzi kutoka mikononi mwa wanajihadi haikua imepangwa.

Kwa mujibu wa serikali ya Ufaransa, wanajihadi wawili wameuawa katika operesheni hiyo na wengine wawili wamejisalimisha. kundi la watu hao wanne ndio walikua wakimshikilia raia huyo wa Uholanzi.

Rais wa Ufaransa ambaye yuko ziarani Izieu, amekaribisha juhudi ya vikosi maalum vya Ufaransa kwa kazi nzuri waliyofanya ya kuangamiza kundi hilo lakini pia kumpata akiwa hai raia wa Uholanzi ambaye alikua akishikiliwa mateka na kundi hilo tangu Novemba 25 mwaka 2011.

Hollande pia amesema ilikuwa "kwa ajili yetu, kwa vikosi vyetu, kupigwa na mshangao kwa kuweza kumuokoa mateka huyo kwa sababu tulikuwa hatuna taarifa yoyote juu ya uwepo wa mateka wa Uholanzi ".