SUDAN - UASI

Waasi wa Kordofan wathibitisha kuliteka lori la vifaa yva kupigia kura

eneo la Kordofan lenye kukumbw ana mzozo wa kivita tangu kipindi kadhaa
eneo la Kordofan lenye kukumbw ana mzozo wa kivita tangu kipindi kadhaa Reuters/Mohamed Nureldin Abdallah

Waasi wa jimbo la Kordofan Kusini nchini Sudan wamethibitisha kwamba wameliteka lori lililokuwa likibeba vifaa vya kupigia kura kwenye uchaguzi unaotarajiwa kupigwa juma lijalo na hivyo kuvuruga uchaguzi katika eneo hilo lenye mzozo wa kivita.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Kundi la ukombozi wa wananchi wa Sudan (SPLM-N) Arnu Lodi amesema wameweka mtego na kuliteka lori lililokuwa limebeba vifaa vya kupigia kura katika barabara inayounganisha mji wa Kdugli mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kusini pamoja na mji wa Dilling.

Hata hivyo msemaji wa jeshi la Sudan kanali Al-Sawarmy Khaled Saad ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kwamba hana taarifa yoyote kuhusu mtego huo.

Mwezi uliopita kundi hilo la SPLM-N lilitangaza dhamira yake ya kuvuruga uchaguzi mkuu wa rais na wabunge unatarajiwa kufanyika April 13, uchaguzi ambao umesusiwa na vyama mashuhiri vya upinzani katika uchaguzi unaotarajiwa kumuona Al Bashir akiendelea kusalia madarakani.

Machafuko yameonekana kushika kasi katika kipindi chote hiki katika jimbo la Kordofan Kusini na katika jimbo jirani la Bleu Nile. Mapigano tangu mwanzoni mwa mwezi March yamesababisha takriban watu elfu ishirini kuyatoroka makwao.

Ijumaa Juma lililopita waziri wa ulinzi Abdel Rahim Mohammed Hussein alieleza kwamba jeshi halitowapa nafasi waasi kuvuruga mchakato wa uchaguzi. Serikali ya kharthoum inakusanya majeshi katika jimbo hilo tangu mwaka 2011 kukabiliana na waasi Kordofan Kusini na Bleu Nile wanaodai kubaguliwa na serikali ya inayoongozwa kwa kiasi kikubwa na watu wenye asili ya warabuni.

Kitengo cha kisiasa cha kundi la SPLM-N ni miongoni mwa vyama vilivyotia sahihi mweszi Desemba iliopita dhidi ya kampeni ya kumshinikiza rais Bachir mwenye umri wa miaka 71 madarakani tangu mwaka 1989 kupitia mapindizu ya kijeshi kung'atuka madarakani.