DRC-JAMII-USALAMA-HAKI

Serikali ya DRC yakiri kuwazika watu katika kaburi la pamoja

Wilaya ya Maluku ambapo walixikwa zaidi ya watu 420.
Wilaya ya Maluku ambapo walixikwa zaidi ya watu 420. Domaine public/Vberger

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekiri Jumatatu wiki hii kuwazika watu 424 katika kaburi la pamoja kwenye kitongoji cha Maluku kilomita mia moja na mji mkuu wa Kinshasa usiku wa tarehe 19 mwezi Machi mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya 400 wanakisiwa kuwa waliuawa na kuzikwa katika makaburi ya Maluku, kilomita 100 na mji wa Kinshasa.

Sakata hili linaendelea kuibua masuali nchini Congo ambapo watu kadhaa wameripotiwa kuuawa mwezi Januari uliopita kufwatia maandamano yaliyoandaliwa na vyama kadhaa vya upinzani kupinga kupitishwa kwa sheria mpya ya uchaguzi.

Hata hivyo, serikali imesema kuwa miili hiyo ni ya watu waliofariki wakiwa na maisha duni ambapo familia zao zilishindwa kulipa malipo ya hospitali pamoja na watoto wanaozaliwa wakiwa wamefariki.

Uchunguzi umeanzishwa ili kujua iwapo watu hao waliuawa na vyombo vya dola au watu ambao serikali inataja kuwa walifariki katika mazingira ya kutatanisha, ambao ni kutoka familia duni.

Shirika la kimataifa la haki za binadamu Human Right Watch limeomba uchunguzi wa kina ufanyika.