KENYA-AL SHABAB-MASHAMBULIZI-USALAMA

Wanafunzi wa vyuo vikuu waandamana Nairobi

Mamia ya wanafunzi wameingia katika mitaa ya mji wa Nairobi, huku wakidai : kuimarika kwa usalama, Aprili 7 mwaka 2015.
Mamia ya wanafunzi wameingia katika mitaa ya mji wa Nairobi, huku wakidai : kuimarika kwa usalama, Aprili 7 mwaka 2015. RFI/Sonia Rolley

Siku tano baada ya mauaji katika Chuo kikuu cha Garissa, nchini Kenya, wanafunzi wa vyuo vikuu wameandamana Jumanne wiki hii na kukusanyika kwenye eneo la Uhuru Park.

Matangazo ya kibiashara

Kwa muda wa siku tatu za maombolezo, heshima ya mwisho imetolea leo Jumanne kwa wahanga wa wanamgambo wa Al Shabab.

Jumanne asubuhi wiki hii, mamia ya wanafunzi wameingia katika mitaa ya mji wa Nairobi, huku wakidai : kuimarika kwa usalama.

Mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu wameandamana, huku wakizuia barabara zinazoingia katika mji wa Nairobi. Waandamanaji hao wamekua na mabango, ambayo yameandikwa “ 148 sio tu idadi” ikimaanisha idadi ya watu waliouawa katika Chuo kikuu cha Garissa. Waandamanaji hao wamefanya ibada ya maombi wakiwa wamepiga goti, huku wakisalia kimya kwa muda wa dakika moja kwa kuwakumbuka wahanga hao 148.

Waandamanaji hao wametoa ujumbe mkali kwa serikali wakisema : “ Tumeuawa, na serikali inafanya nini ?”, amesema mmoja kati ya viogozi wa waandamanaji hao.

Wanafunzi wa vyuo vikuu mjini Nairobi wamepandwa na hasira tangu mwishoni mwa juma lililopita. Jumapili mwishoni mwa juma lililopita, maandamano kama hayo yalishuhudiwa.

Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Nairobi wanabaini kwamba serikali ingelipaswa kuimarisha usalama katika mabweni yote, kwa kuwaweka askari polisi. Wakati huohuo mabweni ya vyuo vikuu yanalindwa na walinzi wa usalama kutoka makampuni ya kibinafsi, ambao, kwa mujibu wa wanafunzi hawana uwezo wa kukabiliana na mashambulizi ya Al Shabab.

Wakati huohuo wahangza wameanza kutambuliwa katika chumba cha kuhifadhi maiti lakini inachukua muda. Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha urasibu wa majanga aliahidi kuwa mchakato wa kuwatambua wahanga utamalizika haraka iwezekanavyo. Mpaka Jumanne asubuhi wiki hii, wahanga 113 ndio walikiua wamesha tambuliwa. 34 wametambuliwa na familia zao. Zaidi ya wahanga 50 wengine waliweza kutambuliwa kwa njia ya alama za vidole na hatimaye 15 kwa njia ya kisasa ya biometriska.