ARFIKA-AFRIKA KUSINI-IS-USALAMA

Afrika Kusini : msichana akamatwa kabala ya kujiunga na IS

Wakati dunia ikiendelea kushuhudia wimbi kubwa la ongezeko la vijana wanaosafiri kwenda nchini Syria na Iraq kujiunga na kundi la Islamic State, bara la Afrika linaelezwa kuwa hatarini zaidi kwa vijana wake kujiunga na kundi hilo.

Msichana mwenye umri wa miaka 15 alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Cape Town, Afrika Kusini, wakati alipokua akijaribu kujiunga na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.
Msichana mwenye umri wa miaka 15 alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Cape Town, Afrika Kusini, wakati alipokua akijaribu kujiunga na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu. myLoupe/Universal Images Group via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati huu ambapo vyombo vya usalama nchini Afrika Kusini juma hili vimefanikiwa kumkamata raia wake wa kike aliyekuwa akijaribu kusafiri kuelekea nchini Syria kupitia Uturuki kujiunga na kundi hilo.

Polisi wamebaini kuwa alikuwa akiwasiliana kwa njia ya mtandao akisoma itikadi za kundi hilo.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa kuna haja ya jumuiya ya kimataifa kutatua tatizo la ukosefu wa ajira duniani ambalo kwa sehemu kubwa ndilo linalochangia vijana kujiunga na makundi haya.

Vijana wengi kutoa bara la Ulaya Marekani na Asia wamejiunga na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu, linaloshikilia baadhi ya maeneo ya Iraq na Syria.
Hivi karibuni kundi hili liliwateka nyara zaidi ya Wakurdi 300, ambao wamekua wakijielekeza katika mji wa Allepo.