Mjadala wa Wiki

Mashambulizi ya kigaidi dhidi ya chuo kikuu cha Garissa kaskazini mashariki mwa Kenya, na hatua mpya

Sauti 12:36

Katika Mjadala wa wiki tunazungumzia Shambulio la kigaidi lililotekelezwa na kundi la wapiganaji wa al Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa kaskazini mashariki mwa Kenya ambapo wanafunzi wasiopungua 150 waliuawa, lakini pia maandamano yaliyofanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu wakishirikiana na wenzao wa Garissa.Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka kusikiliza makala haya, waalikwa ni Brian Wanyama mhadhiri katika chuo kikuu cha kibabii cha mjini Bungoma nchini Kenya, lakini pia francis Onditi, ni mchambuzi wa kisiasa, na mtaalamu wa masuala ya usalama akiwa Nairobi nchini Kenya.