UFARANSA-RWANDA-MAUAJI-USALAMA-HAKI

Ufaransa yakana kuhusika katika mauaji ya kimbari ya Rwanda

Ikulu ya Ufaransa ya Elysee imetangaza hapo jana kuweka bayana nyaraka za kiulinzi, kiusalama na kidiplomasia baina ya nchi hiyo na Rwanda kwa kipindi cha mwaka 1990 hadi 1995.

Wanajeshi wa Ufaransa wakiwasili karibu na mji wa Butare, Rwanda, Julai 3, 1994, siku kumi baada ya koperesheni Turquoise kunza.
Wanajeshi wa Ufaransa wakiwasili karibu na mji wa Butare, Rwanda, Julai 3, 1994, siku kumi baada ya koperesheni Turquoise kunza. HOCINE ZAOURAR / ARCHIVES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imechukuliwa siku ya maadhimisho ya miaka 21 ya kuzuka kwa mauaji ya kimbari tarehe 7 mwezi Aprili 7 mwaka 1994 nchini Rwanda.

Nia ya serikali ya Ufaransa ni kuonyesha kuwa nchi hiyo haikushiriki katika mauaji hayo tofauti na alivyodai rais Paul Kagame wa Rwanda mwaka uliopita, lakini pia kuleta maridhiano na ushirikiano mzuri wa kidiplomasia pamoja na uungwana wa viongozi wa Ufaransa.

"Rais wa Ufaransa François Hollande alitangaza mwaka mmoja uliopita kwamba Ufaransa itafanya kilio chini ya uwezo wake ili kuweka uwazi na kuwezesha kazi ya kumbukumbu kuhusu kipindi hicho bila hata hivyo kuweka wazi uamzi huu", wamesema washauri wa rais Hollande. Tangu wakati huo, sensa ya nyaraka za zamani "ilizinduliwa na kufanyiwa na uratibu" na Sekretarieti kuu ya Ulinzi wa taifa na Usalama (SGDSN), nyaraka zilio na maelezo ya washauri wa kidiplomasia na kijeshi wa Ikulu ya Elysée, lakini pia ripoti ziliotolewa na ushauri mdogo wa mikutano ya ulinzi au vikao baina ya wizara.