SENEGAL-SIASA

Macky Sall mbioni kutekeleza ahadi zake

Rais wa Senegal, Macky Sall alipokua akiendesha kampeni za chama chake, aliahidi kupunguza muhula wake kutoka miaka saba hadi miaka 5.

Rais wa Senegal, Macky Sall, Machi 17 mwaka 2014.
Rais wa Senegal, Macky Sall, Machi 17 mwaka 2014. .RFI/Carine Frenk
Matangazo ya kibiashara

Wakti huo alitangaza kura ya maoni kuhusu suala hili ifikapo mwezi mei mwaka 2016, lakini mvutano umeanza kujitokeza katika chama chake cha APR, huku baadhi ya wafuasi vigogo wa chama hicho tawala, wakipinga mageuzi hayo.

Msemaji wa serikali Oumar Youm amethibitisha kwamba katika sekta ya uchumi, siasa na Katiba mageuzi hayo “hayakupewa nafasi”.

Wadadisi wengi kutoka Senegal, wamebaini kwamba wakati rais akiwa pia kiongozi wa chama chake cha APR alipotangaza kuhusu suala hilo, mjadala na mvutano havingipaswa kuwepo baina ya wafuasi wa chama hicho.

“ Kwanini rais hachukui uamzi wa kukomesha malumbano hayo katika chama chake, au huenda ni mbinu anazotumia ili kurejelea kauli yake”, amejiuliza Babacar Justin, mmoja kati ya waaandishi wa habari wa Senegal, huku akibaini kwamba, kuongeza au kupunguza muhula ni kwenda kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Mmoja wa washiriki wa rais Macky Sall amethibitisha kwamba rais ameamua kuheshimu ahadi yake, laakini anatambua kwamba haungwi mkono na wengi miongoni mwa wafuasi wa chama chake.

“ Mjadala uko mbioni kumalizika, kwani rais alikula kiapo kwamba ataheshimu Katiba ya nchi”, chanzo hiki kimeonya. Ni vigumu chama cha APR kutolea wito wafuasi wake kupiga kura ya hapana, iwapo kura ya maoni itaitishwa.

“ Vipi chama kitajivua imani kwa kiongozi wake wakati ni ahadi aliyoitoa mara kadhaa?”. Amejiuliza mkurugenzi wa gazeli la kila wiki la Nouvel Horizon, Issa Sall.