RWANDA-UFARANSA-DIPLOMASIA

Rwanda yapongeza hatua ya Ufaransa

Picha za wahanga ziliyotundiikwa kwenye eneo la kumbukumbu la mauaji ya kimbari, Kigali, Rwanda.
Picha za wahanga ziliyotundiikwa kwenye eneo la kumbukumbu la mauaji ya kimbari, Kigali, Rwanda. REUTERS/Noor Khamis

Raia wengi wa Rwanda bado wana dukuduku ya kufahamu kiliyomo katika nyaraka ziliyowekwa bayana na Ikulu ya Elysée nchini Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Nyaraka hizo zinahusu mahusiano ya Ufaransa na Rwanda kati ya mwaka 1990 na 1995, ikimaanisha kabla, wakati na baada ya mauaji ya kimbari. Serikali ya Rwanda imekaribisha uamzi huo, huku ikionesha baadhi ya tahadhari.

Uhusiano kati ya Ufaransa na Rwanda umeendelea kudorora. Rais wa Rwanda Paul Kagame anaituhuma Ufaransa kuwa ilishiriki katika utekelezaji wa mauaji ya kimbari, tuhuma ambazo Ufaransa inafutiliwa mbali. Waziri wa Sheria wa Ufaransa amesema ana imani kwamba kuwekwa bayana kwa nyaraka hizo kutafufua mahusiano kati ya nchi hizi mbili.

Ikulu ya Elysée na serikali ya Rwanda hazikufahamishwa kuhusu kuwekwa bayana kwa nyara hizi. " Hii haiuhusu Kigali, hatua hii sio ya kidiplomasia", wamesema washirika wa karibu rais François Hollande. Kuwekwa bayana kwa nyaraka hizi kunakwenda sambamba na mtazamo wa kihistoria na kumbukumbu ya rais wa Ufaransa.

Baadhi ya wakaazi wa kitongoji cha Kamuhanda, moja ya vitongoji vya Kigali, wamenyooshea kidolea cha lawama jeshi la Ufaransa kwamba lilishiriki katika mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994, hasa kuwatolea mafunzo ya kijeshi wanamgambo wa "Interahamwe" wa chama cha Juvenal habyarimana cha MRND.

Hatua ya Ufaransa ya kuweka bayana nyaraka za kiulinzi, kiusalama na kidiplomasia baina ya nchi hiyo na Rwanda kwa kipindi cha mwaka 1990 hadi 1995 ilichukuliwa siku ya maadhimisho ya miaka 21 ya kuzuka kwa mauaji ya kimbari tarehe 7 mwezi Aprili 7 mwaka 1994 nchini Rwanda.

Nia ya serikali ya Ufaransa ni kuonyesha kuwa nchi hiyo haikushiriki katika mauaji hayo tofauti na alivyodai rais Paul Kagame wa Rwanda mwaka uliopita, lakini pia kuleta maridhiano na ushirikiano mzuri wa kidiplomasia pamoja na uungwana wa viongozi wa Ufaransa.

" Rais wa Ufaransa François Hollande alitangaza mwaka mmoja uliopita kwamba Ufaransa itafanya kilio chini ya uwezo wake ili kuweka uwazi na kuwezesha kazi ya kumbukumbu kuhusu kipindi hicho bila hata hivyo kuweka wazi uamzi huu", wamesema washauri wa rais Hollande. Tangu wakati huo, sensa ya nyaraka za zamani "ilizinduliwa na kufanyiwa na uratibu" na Sekretarieti kuu ya Ulinzi wa taifa na Usalama (SGDSN), nyaraka zilio na maelezo ya washauri wa kidiplomasia na kijeshi wa Ikulu ya Elysée, lakini pia ripoti ziliotolewa na ushauri mdogo wa mikutano ya ulinzi au vikao baina ya wizara.