UGANDA-MAUJI-UGAIDI-USALAMA

Mauaji ya Joan Kagezi Uganda : watuhumiwa kadhaa wakamatwa

Watuhumiwa kadhaa wamekamatwa kufuatia uchunguzi wa mauaji ya Joan Kagezi, Mwendesha mashtaka aliyeuawa Machi 30 mwaka 2015 katika mji wa kampala, nchini Uganda.

Eneo Mwendesha mashtaka, Joan Kagezi, alikouawa na watu aliokua kwenye pikipiki, Machi 31 mwaka 2015 katika kitongoji  cha Kampala
Eneo Mwendesha mashtaka, Joan Kagezi, alikouawa na watu aliokua kwenye pikipiki, Machi 31 mwaka 2015 katika kitongoji cha Kampala AFP PHOTO/ ISAAC KASAMANI
Matangazo ya kibiashara

Joan Kagezi alikua akisimamia kesi ya mashambulizi ya wanamgambo wa kiislamu ya mwaka 2010. Mmoja wa Watuhumiwa ni mfungwa wa zamani katika jela la Guantanamo.

Jamal Kiyemba, raia wa uganda aliyekua akiishi Uingereza, aliachiliwa huru kutoka katika jela hilo mwaka 2006, baada ya kukamtwa nchini Pakistan mwaka 2002, akishukiwa kushirikiana na kundi la Al Qaeda, lakini hakuweza kupatikana na hatia. Baada ya kuachiliwa huru, Jamal Kiyemba, alitumwa Uganda.

Marekani ilishiriki katika operesheni ya kuwakamata watuhumiwa hao, amethibitisha msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Marie Harf.

Kwa mujibu wa viongozi wa Uganda takriban watu sita ikiwa ni pamoja na wanawake wawili na wanaume wanne walikamtwa hivi karibuni.

Hata hivyo mwishoni mwa mwezi Machi, polisi ya Uganda ilieleza kwamba haijamkamata mtuhumiwa hata mmoja na kubaini kwamba hawana taarifa yoyote kuhusu watu waliohusika katika mauaji ya Joan Kagezi. Naibu huyo kiongozi wa Mashitaka aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wawili waliokua kwenye pikipiki Machi 31 mwaka 2015.