Serikali ya Kenya kufunga akaunti za fedha za watu 85, kugundulika kwa kaburi la pamoja DRC, na Ufaransa kujiapiza kupinga ugaidi Afrika Mashariki
Imechapishwa:
Cheza - 21:39
Taifa la Kenya juma hili lililogubikwa na simanzi kufwatia vifo vya wanafunzi mia arobaini na tisa, waliouawa katika shsmbulizi la kigaidi lililotekelezwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab dhidi ya chuo kikuu cha Garisa, kaskazini mashariki mwa Kenya,Kufwatia hali hiyo serikali ilichukua hatua ya kuzifunga akaunti za watu 85, na makampuni 13 ya usafirishaji wa pesa.Huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Serikali ilikiri kuwazika watu 424 katika kaburi la pamoja kwenye kitongoji cha Maluku kilomita mia moja na mji Mkuu wa Kinshasa usiku wa tarehe 19 Mwezi Machi mwaka huu.Ufaransa kwa juma hili imesema iko tayari kupambana na ugaidi, katika eneo la Afrika Mashariki.