GABON-UPINZANI-KIFO-SIASA

Gabon : machafuko yatokea baada ya kifo cha André Mba Obame

Kiongozi wa upinzani Gabon, André Mba Obame katika uwanja wa ndege wa Leon Mba wa Libreville, Desemba 30 mwaka 2010.
Kiongozi wa upinzani Gabon, André Mba Obame katika uwanja wa ndege wa Leon Mba wa Libreville, Desemba 30 mwaka 2010. Wils Yanick Maniengu /AFP

Makabiliano baina ya Polisi na wafwasi wa chama cha Upinzani cha “Union Nationale” cha André Mba Obame, nchini Gabon yametokea Jumapili mwishoni mwa Juma hili mjini Libreville kufwatia kifo cha kinara kinara huyo aliyefariki mjini Yaounde nchini Cameroon.

Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa chama cha Union nationale wamechoma moto magari na majengo kadhaa kuonyesha gadhabu yao, yakiwemo majengo ya balozi za Benin, Nigeria, Cameroon na kadhalika, jambo ambalo linakemewe na Ikulu ya Gabon kwa vile kifo cha mpinzani huyo ni kufwatia ugonjwa.

André Mba Obame, kinara wa upinzani wa Gabon na mwasisi wa chama Umoja wa kitaifa (Union nationale) alifariki Jumapili mwishoni mwa juma hili nchini Cameroon, ambapo alikua akitibiwa kwa siku kadhaa.

Mba Obame alikua waziri katika utawala wa Omar Bongo, baba wa rais wa sasa wa Gabon, Ali Bongo, na alijiunga na upinzani mwaka 2009. Mba Obame alikua mmoja kati ya viongozi wakuu wa pinzani tangu kupingwa kwa uchaguzi wa rais Ali Bongo, baada ya kifo cha babake.

André Mba Obame, amefariki akiwa na umri wa mika 57 na a upinzani umebaini kwamba umempoteza mtu maarufu kwao.

Kifo cha kinara huyo wa upinzani nchini Gabon kilitokea Jumapili mchana nchini Cameroon, na alikua anatazamiwa kusafirishwa nchini Afrika Kusini, ambapo angeliendelea kupata huduma za matibabu, amesema mwipwa wake François Ondo Edou, katibu mtendaji wa chama cha Union nationale. Baaada ya afya yake kuwa mbaya zaidi, André Mba Obame alisafirishwa hadi hospitali ambapo alifariki

“ Sote tunafahamu kwamba André Mba Obame, alikua mgonjwa tangu Uchaguzi wa urais wa mwaka 2009, ambao aliibuka mshindi. Alikua Afrika Kusini ambapo alifanyiwa upasuaji na baadae alisafiri Ufaransa na kurejea hapa nchini. Lakini hata hivyo afya yake iliendelea kuwa mbaya. Na ndio sababu iliyompelekea asafiri nje ya nchi ili aweze kutibiwa”, amesema François Ondo Edou.

André Mba Obame alichukua nafasi ya tatu katika uchaguzi wa mwaka 2009, uchaguzi ambao Ali Bongo aliibuka mshindi, kulingana na matokeo rasmi yaliotangazwa na Mahakama ya Katiba. Hata hivyo André Mba Obame alitangaza alishinda uchaguzi huo na kujitangza rais mteule.