SUDAN-UCHAGUZI-UPINZANI-SIASA

Sudan : Uchaguzi usiokua na ushindani wala upinzani

Takriban watu milioni 13 nchini Sudan wanatarajiwa kupiga kura kuanzia hii Jumatatu wiki hii kumchagua rais wao, lakini pia wabunge na wakuu wa mikoa.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati wa kampeni,  Aprili 9 mwaka 2015.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati wa kampeni, Aprili 9 mwaka 2015. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu unatazamiwa kufanyika kwa muda wa siku tatu

Rais Omar al-Bashir anatarajiwa kushinda uchaguzi huo bila upinzani mkubwa kwa vile wapinzani wakuu kama Hassan al-Tourabi na Sadeq Al Mahdi wamesusia uchaguzi huo kwa madai ya kuwepo kwa uchakachuaji kuandaa ushindi wa rais Omar al-Bashir aliyeko madarakani kwa zaidi ya miaka 25.

Omar al-Bashir yuko madarakani kwa kipindi cha miaka 26 sasa, na anagomea muhula mwengine wa miaka mitano.

Kama ilivyokuwa mwaka 2010, vyama vya upunzani vimesusia uchaguzi huu. Na hakuna mgombea mwenye ushawishi mkubwa kwa wananchi, ambaye anaonekana kuwa atamshinda Omar al-Bashir.

Hata hivyo wagombea kumi na watano ambao wanashiriki kinyang'ayiro hiki cha urais dhidi ya Omar al-Bashir wanaonekana kuwa wanafanya mazoezi bila hata hivyo kujali mashahi ya taifa na ya wananchi.

Wakati huohuo jumuiya ya kimataifa pamoja na Umoj awa Ulaya wamesema hawana imani na uchaguzi huu, wakibaini kwamba demokrasia imeendelea kukumbwa na kizungumkuti nchini Sudani.

Utawala unamatumaini kwamba baada ya uchaguzi huu, mazungumzo ya kisiasa yaliyopendekezwa na upinzani mwaka mmoja uliyopita, yanaweza yakaanza. Mwezi Desemba mwaka 2014, makundi mbalimbali ya watu wenye silaha na vyama vya kisisasa vya upinzani, ikiwa ni pamoja chama cha Ouma, waliweka saini kwenye mkataba waliouita ” Wito kwa Sudan”. Lengo la mkataba huo ilikua kuuangusha utawala wa Omar al-Bashir.