UN-KENYA-WAKIMBIZI-SOMALIA-USALAMA

UN haijapokea maombi kutoka serikali ya Kenya

Kambi ya wakimbizi wa Somalia ya Dadaab, ambayo serikali ya Kenya inataka ifungwe kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi ya Al Shabab.
Kambi ya wakimbizi wa Somalia ya Dadaab, ambayo serikali ya Kenya inataka ifungwe kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi ya Al Shabab. © Natasha Lewer / MSF

Tume ya Umoja wa Mataifa inayowashughulikia wakimbizi UNHCR inasema haijapokea maombi rasmi kutoka kwa serikali ya Kenya, kuwarudisha nyumbani wakimbizi raia wa Somalia wanaoishi katika kambi ya Daadad Kaskazini Mashariki mwa Somalia.

Matangazo ya kibiashara

Naiorbi inataka wakimbizi hao kurudi nyumbani kwa muda wa miezi mitatu ijayo kwa kile inachosema kambi hiyo inatumiwa kupanga na kutoa mafunzo ya kigaidi.

Serikali ya Kenya imesisitiza kuwa wakimbizi raia wa Somalia wanaoishi katika kambi ya Daadad watahamishwa katika nchi yao kwa muda wa miezi mitatu ijayo.

Naibu rais William Ruto amesema hatua hiyo inachukuliwa kama njia mojawapo ya kupambana na ugaidi, baada ya kubainika kuwa kambi hiyo imekuwa ikitumiwa kutoa mafunzo kwa wanamgambo wa Al Shabab kutoka Somalia.

Ruto ameongeza kuwa jeshi la Kenya halitaondoka Somalia kama linavyotaka kundi la kigaidi la Al Shabab ambalo lilishambulia Chuo Kikuu cha Garrisa majuma mawili yaliyopita na kusababisha vifo vya watu 148, ikiwa ni pamoja na wanafunzi 142.

Al Shabab imekuwa ikisema inaishambulia Kenya kwa sababu imeakataa kuondoa wanajeshi wake nchini Somalia na kutishia kutekeleza mashambulizi zaidi.