DRC-SHERIA-USALAMA

Kesi ya Vital kamerhe yaahirishwa

Kiongozi wa chama cha upinzani cha UNC Vital Kamerhe.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha UNC Vital Kamerhe. AFP PHOTO/ ADIA TSHIPUKU

Mahakama mjini kinshasa Kwa mara nyingine imeiahirisha Kesi inayomkabili kiongozi wa chama cha upinzani cha UNC Vital Kamerhe.

Matangazo ya kibiashara

Vital Kamerrhe anakabiliwa na tuhuma za kufanya udanganyifu wa kura dhidi ya mwanasiasa kutoka vyama vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila, bi Wivine Moleka.

Hayo yakijiri hali ya utulivu imerejea mtaani Rutshuru jimboni Kivu ya kaskazni mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, baada ya mamia kwa maelfu ya wananchi kufanya maandamano ya kupinga kuuawa kwa raia mmoja wa kawaida na kikosi cha kulinda amani, Monusco mjini Nyamilima, mashariki mwa nchi hiyo.

Mwenyekiti wa mashirika ya kiraia wilayani Rutshuru, mashariki mwa nchi hiyo, Jean Claude Mbabaze amesema kuwa maafisa wa kikosi cha Umoja wa Mataifa, hawakuwa na nia ya kumuuwa mtu huyo, wakibani kwamba tukio hilo limetokea tu kwa bahati mbaya.