AFRIKA KUSINI-HAKI-USALAMA

Serikali ya Afrika kusini yatoa onyo kwa raia wake

Serikali ya Afrika Kusini inakemea vikali vitendo vya kuwanyanyasa na kuwaua wageni nchini humo vinavyoendelea kujitokeza na kutishia usalama wa watu wasio na hatia.

Timu ya maafisa wa usafi ya Manispaa ya Durban baada ya vijana wa Afika kusini kupora doka moja la mfanyabishara kutoka Somaliai, Durban, Aprili 10 mwaka 2015.
Timu ya maafisa wa usafi ya Manispaa ya Durban baada ya vijana wa Afika kusini kupora doka moja la mfanyabishara kutoka Somaliai, Durban, Aprili 10 mwaka 2015. AFP/RAJESH JANTILAL
Matangazo ya kibiashara

Onyo hilo inakuja wakati mashambulizi dhidi ya wageni yanaendelea kutekelezwa mji wa Durban baada ya mfalme wa jamii ya Zulu Goodwill Zwelithini kutoa wito kwa wageni kukunja jamvi zao na kuondoka nchini humo.

Hata hivyo, katika mkutano na waandishi wa habari, mawaziri kadhaa wameonya Jumanne wiki hii dhidi ya unyanyasaji huo wakibainisha kuwa nchi ya Afrika Kusini imetia saini kwenye Itifaki zinazohusiana na hadhi ya wakimbizi.

Waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa, amerejelea wito uliyotolewa na rais wa nchi hio Jacob Zuma wa kuwataka raia wa Afrika Kusini wanao jihusisha na tabia ya kuwabagua na kuwafanyia vitendo viovu raia wa kigeni kuachana na tabia hio mara moja, la sivyo watachukuliwa hatu za kisheria.

Raia wanne wa kigeni ndio wanaripotiwa kuuawa na raia wa Afrika Kusini tangu vurugu hizo zilipoanza.