AFRIKA-LIBYA-ITALIA-WAHAMIAJI-AJALI

Hali ya kutisha ya kufa maji kwa watoto katika ajali za baharini

Jumatano wahamiaji 48 walitia nanga katika mji wa Palermo, Sicile, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, na kupelekea idadi ya wahamiaji 1,500 waliopkelewa katika bandari hii ndani ya saa 24.
Jumatano wahamiaji 48 walitia nanga katika mji wa Palermo, Sicile, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, na kupelekea idadi ya wahamiaji 1,500 waliopkelewa katika bandari hii ndani ya saa 24. REUTERS/Guglielmo Mangiapane

Hali ya wasiwsi imeendelea kutanda kuhusu hatima ya wahamiaji 400 waliokufa maji katika Bahari ya Medieterranean mwishoni mwa juma lililopita.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kuhusu kuzama kwa meli iliyokua ikibeba wahamiaji haramu ilitolewa na mtu aliyenusurika baada ya kuokolewa na timu ya walinzi wa bahari upande wa Italia.

Shirika linalotetea haki za watoto Save the Children limekusanya baadhi ya taarifa zinazoonekana kuthibitisha tukio hilo la kuzama kwa meli iliyokua imebeba watu 500, ikiwa ni pamoja na watoto.

"Janga kwa wahamiaji hawa, hasa vijana, limeanza kabla ya kupanda meli na kuvuka Mediterranean. Safari kwa meli ni ushahidi mwingine wa ziada ambao unakuja baada ya matukio mengi ya kutisha yaliyoshuhudiwa kati ya nchi wanakotoka wahamiaji na Libya", msemaji wa shirika Save the Children, Michele Prosperi ameielezea RFI, huku akibani kwamba wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kuzama kwa meli hiyo.

" Kulingana na taarifa tulizo nazo, wahamiaji hao wamekua wakisafirishwa na wafanyabiashara haramu ya madawa ya kulevya, ambao wamekua wakiwapiga kwa aina yoyote, huku wengine wakipata mateso, na baadhi yao wamekua wakichomwa moto wakiwa hai mbele ya macho ya wengine", ameongeza Prosperi.

Miongoni mwa manusura 150 waliohojiwa baada ya kuokolewa, watano ni watoto. Inasemekana kwamba vijana na watoto ni miongoni mwa wahamiaji waliokufa maji katika ajali hio.