DRC-MAUAJI-USALAMA

DRC : zaidi ya watu 15 wauawa Mambasa

Zaidi ta watu kumi na tano wameuawa na wengine kuchukuliwa na watu wanaosadiki wa kuwa wapiganaji wa kijadi wa kundi la Mai mai Simba wakishirikiana na waasi wa Uganda wa ADF-Nalu.

Desemba 3 mwaka 2014. Beni, Kivu Kaskazini, DR Congo: Askari wa Jeshi la DR Congo wakipiga doria katika mji wa Beni dhidi ya mashambulizi ya makundi yenye silaha.
Desemba 3 mwaka 2014. Beni, Kivu Kaskazini, DR Congo: Askari wa Jeshi la DR Congo wakipiga doria katika mji wa Beni dhidi ya mashambulizi ya makundi yenye silaha. MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo inasadikiwa kuwa kundi la Mai mai Simba lilishambulia vijiji viwili vya Elota na Mabutua wilayani Mambasa, katika mkoa wa Mashariki unaofahamika kama Province Orientale.

Wapiganaji hao walivamia vijiji hivyo, Alhamisi Aprili 16, wiki moja baada ya jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwatokomeza wapiganaji hao kwenye maeneo hayo.

Taarifa zaidi zinasema wapiganaji hao walijifananisha na wanajeshi wa serikali wanaokuja kulinda usalama wa wananchi katika vijiji hivyo, na mara baada ya kuwasili kwao kuanzia kijiji cha Sowuma, walimkamata raia mmoja na kumkata kichwa.

Hayo yakijiri Tume ya " Haki na Amani" ya Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imezindua Alhamisi wiki hii mpango wake wa kutoa mafunzo kwa wachunguzi wa uchaguzi maarufu kwa lugha ya Lingala kama " Bokengi Bwa maponomi, BBM".

Mpango huo unaofadhiliwa na serikali ya Marekani unalenga kusaidia kujenga hali ya maridhiano na kuimarisha uwezo wa Kanisa kuchunguza uchaguzi wa mwaka 2016 kwa viwango vya kimataifa vya uwazi na uaminifu.