AFRIKA-LIBYA-ITALIA-WAHAMIAJI-AJALI

Wahamiaji wa Kiislamu watuhumiwa kuwatupa Wakristo baharini

Polisi ya Italia imewakamata wahamiaji kumi na tano kutoka Afrika ambao wanashukiwa kuwatupa baharini wahamiaji wenzao ambao ni Wakristo waliokua wakishirikiana safari.

Wahamiaji katika bandari ya Palerme, Aprili 15 mwaka 2015.
Wahamiaji katika bandari ya Palerme, Aprili 15 mwaka 2015. REUTERS/Guglielmo Mangiapane
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo zaidi ya wahamiaji wengine arobani wamekufa maji baada ya meli yao kuzama wakati ilipokua ikijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean. Mamia ya wahamiaji walionusurika wamewasili siku za hivi karibuni katika mji wa Reggio Calabria, nchini Italia, wengi wao ni kutoka nchi za kusini mwa Sahara

Kulingana na ushahidi wa manusura tisa wa dini ya Kikristo, walionukuliwa na vyombo vya habari vya Italia, wahamiaji 105, wengi wao wakiwa ni kutoka Senegal na Côte d’Ivoire ambao ni Waislamu waliondoka pwani ya Libya Aprili 14 wakiwa wamejazana kwenye sehemu kulikokuwa kuliwekwa matairi. Wakati walipokua wakivuka bahari ya Mediterranean, rabsha ilitokea kati ya Waislamu na Wakristo.

Wahamiaji kutoka Nigeria, Ghana na Mali walitishiwa mara kadhaa kutupwa baharini kutokana na " dini yao ya Ukristo ”. “ Chanzo cha uhasama wao kinatokana na dini” polisi imesema.

Inaarifiwa kuwa wakati wa usiku, Waislamu kumi na tano walichukuliwa hatua ya kutupa Wakristo kumi na mbili katika mawimbi, katika maji ya kimataifa. Wahamiaji wengine Wakristo hawakuweza kunusurika na baadae walikufa maji.

Meli, ambayo ilikuwa katika matatizo katika pwani ya Sicily, iliokolewa na manuari ya Italia na wakati abiria walipowasili katika mji wa Palerme, Wakristo walisikilizwa na Ofisi ya mashataka ya Palerme. Watuhumiwa kumi na tano waliohusika na kitendo cha kuwatupa wenzio baharini walikamatwa na kufungwa kwa tuhuma za mauaji yenye misingi ya kidini. Polisi ya Palerme imesema kuwa watuhumiwa hao ni raia kutoka Côte d’Ivoire, Mali na Senegal.