BURUNDI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lawaonya wanasiasa wa Burundi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaitaka serikali ya Burundi na wanasiasa wa upinzani, kuepuka matamshi yanayoweza kusababisha machafuko nchini humo kuelekea ,wakati na baada ya Uchaguzi wa urais mwezi Juni mwaka huu.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe hao 15 wameongeza kuwa vitisho vinaweza kusababisha hali kuwa mbaya hasa wakati huu ambapo tayari zaidi ya watu elfu nane wamekimbilia nchini Rwanda kwa hofu ya kuzuka kwa machafuko machafuko.

Burundi pia imetakiwa kuhakikisha kuwa kuna mazingira mazuri ya uchaguzi huo kufanyika kwa njia ya amani, na zoezi hilo linakuwa huru na haki.

Siku ya Ijumaa, polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya na kuzuia maandamano ya upinzani jijini Bujumbura kumshinikiza rais Piere Nkurunza kutowania urais kwa muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza Burundigvt
Maandamano jijini Bujumbura
Maandamano jijini Bujumbura