AFRIKA KUSINI

Wageni waendelea kulengwa nchini Afrika Kusini

Raia wa kigeni waliokimbia makwao
Raia wa kigeni waliokimbia makwao Alexandra Brangeon / RFI

Mataifa jirani na Afrika Kusini yanasema yanajiadaa kuwarudisha nyumbani raia wake baada ya kuendelea kwa uvamizi na uuaji wa raia wa kigeni nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Uvamizi na mauaji haya yalianzia mjini Durban, na tayari raia sita wa kigeni wamepoteza maisha na siku ya Ijumaa na Jumamosi  wamiliki wa maduka jijini Johannesburg walifunga maduka yao kwa hofu ya kuvamiwa.

Uvamizi huo umesabisha maelfu ya watu kukimbia makwao, na Umoja wa Mataifa umelaaani kinachoendelea nchini Afrika Kusini.

UN inasema kwa muda wa wiki tatu zilizopita, raia wa kigeni elfu 5 wameyakimbia makwao na wanaishi katika vituo vya polisi.

Juma hili kulikuwa na maandamano makubwa katika miji mikuu nchini humo kupinga mauaji haya ambayo vijana nchini humo kazi zao zimechukuliwa na wageni.

Raia wa kigeni waliokimbia makwao
Raia wa kigeni waliokimbia makwao Reuters/Rogan Ward

Polisi wakipambana na wavamizi wa raia wa kigeni
Polisi wakipambana na wavamizi wa raia wa kigeni REUTERS/Rogan Ward