ETHIOPIA-MAUJI-USALAMA-HAKI

IS yarusha video inayoonyesha mauaji ya Waethiopia

Wapiganaji wa Islamic State katika mkoa wa Raqqa, Syria, June mwaka 2014.
Wapiganaji wa Islamic State katika mkoa wa Raqqa, Syria, June mwaka 2014. REUTERS/Stringer

Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu limerusha hewani video ambamo linaeleza ushirikiano wake na Ukristo. Wakristo wa Raqqa, makao makuu ya kundi la kijihadi nchini Syria wameeleza kuwa wamekua wakitozwa kodi ili waendelee kuishi mjini humo wakiwa Wakristo.

Matangazo ya kibiashara

Lakini video hiyo ya dakika 29 inamalizika kwa kuwaua zaidi ya raia thelathini wa Ethiopia nchini Libya.

Mwanzo wa filamu hii inaonekana kama tamthilia ya historia. Kundi hilo la wanajihadi wanaanza katika video hiyo kwa kuonyesha Makanisa mbalimbali ya Kikristo: Waumini wa kanisa Katoliki kutoka madhehebu ya Roman Catholic, Wakristo wa Mashariki na Waprotestanti.

Kisha kundi hilo la wanajihadi linaelezea tofauti za kiteolojia kati ya Ukristo na Uislamu. Kundi hili linaeleza utaratibu wa dhimmi, uliyosahihishwa na sheria ya kitamaduni ya Kiislamu kwa watu wasiokuwa Waislamu waishio katika nchi ya kiislamu.

Baada ya kulipa kodi na kukubali kuweka kando baadhi ya haki zao, jamii za watu wachache zinaweza kunufaika na uhuru mdogo wa ibada na ulinzi. Utaratibu ambao kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu linasema kuwa limepitisha kwa watu wasio Waislamu wanaoishi katika maeneo yake. Wakristo wa Raqqa, makao makuu ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu kaskazini mwa Syria, wanaonekana mbele ya kamera na kusema kuwa wamechagua utaratibu huo.

Makundi mawili ya raia wa Ethiopia yalionyeshwa katika picha. Baadhi, wamevaa nguo za rangi ya machungwa ikimaanisha wafungwa wa Guantanamo,wakiwa karibu na bahari kaskazini mwa Libya. Wengine wamevaa suruali na shati vya bluu, huku wakiwa jangwani, katika mkoa wa Fezan nchini Libya, kwa mujibu wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu. Baadhi ya wanajihadi walikua tayari kuwakata vichwa mateka hao, huku wakifunika nyuso zao.

Kisa hiki cha tatu ni, tishio la moja kwa moja la kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu dhidi ya " waumini wa msalaba". Mtu aliyekua alijifunika uso wake aliweka bunduki yake kwenye kamera huku akiongea kwa lugha ya Kiingereza, akiwaeleza Wakristo wa ulimwengu mzima. " Hamtakua na usalama kama hamtakubali Uislamu, aidha kulipa Jizya (kodi) na kukubali kunyeyekea", amesema mtu huyo. Jizya ni kodi ambayo inapelekea watu wasio Waislamu waishio katika nchi ya kiislamu kuwa na uhuru fulani, kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu.

Serikali ya Ethiopia imelaani mauaji ya raia wake zaidi ya thelathini huku ikiapa kupambana na Waislamu wenye itikadi kali za kidini.