AFRIKA KUSINI-UBAGUZI-USALAMA

Zuma ajaribu kuwahakikishia wageni usalama wao

Wahamiaji wakikimbilia katika kambi ya Primrose nje ya mji wa Johannesburg, Aprili 18 mwaka 2015, ili kuepuka mateso na unyanyasaji dhidi ya wageni vinavyoshuhudiwa Afrika Kusini.
Wahamiaji wakikimbilia katika kambi ya Primrose nje ya mji wa Johannesburg, Aprili 18 mwaka 2015, ili kuepuka mateso na unyanyasaji dhidi ya wageni vinavyoshuhudiwa Afrika Kusini. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Nchini Afrika Kusini, mateso na unyanyasaji dhidi ya wageni vimeukumba mkoa mwingine wa Johannesburg. Tangu Jumatano, mji wa Johannesburg na vitongoji vyake vimeedelea kushuhudia vurugu na uporaji dhidi ya maduka ya raia wa kigeni waishio katika mji huo.

Matangazo ya kibiashara

Hali ilikuwa mbaya Jumamosi Aprili 18, hasa katika kitongoji cha Alexandra. Rais Jacob Zuma ameamua kufuta ziara yake Indonesia katika hali ya kukabiliana na suala hili.
Mataifa jirani na Afrika Kusini yanasema yanajiadaa kuwarudisha nyumbani raia wake baada ya kuendelea kwa uvamizi na uuaji wa raia wa kigeni nchini humo.

Uvamizi na mauaji haya yalianzia mjini Durban, na tayari raia sita wa kigeni wamepoteza maisha na siku ya Ijumaa na Jumamosi  wamiliki wa maduka jijini Johannesburg walifunga maduka yao kwa hofu ya kuvamiwa.

Uvamizi huo umesabisha maelfu ya watu kukimbia makwao, na Umoja wa Mataifa umelaaani kinachoendelea nchini Afrika Kusini.

UN inasema kwa muda wa wiki tatu zilizopita, raia wa kigeni elfu 5 wameyakimbia makwao na wanaishi katika vituo vya polisi.

Juma hili kulikuwa na maandamano makubwa katika miji mikuu nchini humo kupinga mauaji haya ambayo vijana nchini humo kazi zao zimechukuliwa na wageni.