ETHIOPIA-IS-MAUJI-USALAMA-HAKI

Ethiopia yalaani mauaji ya raia wake

Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, Januari 26 mwaka 2013.
Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, Januari 26 mwaka 2013. REUTERS/Tiksa Negeri

Baada ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu kutangaza kuwaua zaidi ya Wakristo thelathini kutoka Ethiopia waliotekwa nyara nchini Libya, Ethiopia imelaani mauaji hayo na kuahidi kupambana dhidi ya magaidi.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Ethiopia wamesema kuwa wameiona video iliyokua ikionyesha raia wake wanavyouawa. Msemaji wa serikali ya Ethiopia, Redwan Hussein, amesema mauaji hayo yanatia huzuni, na kusema kuwa serikali ya Ethiopia haitokubali kisa hicho kiendelea.

Wakati huohuo ubalozi wa Ethiopia nchini Misri unajaribu kuthibitisha utambulisho wa raia hao thelathini waliouawa nchini Libya. Inawezekana kuwa ni wahamiaji ambao walitaka kwenda Ulaya. Ethiopia inatazamiwa kutoa maelekezo kwa raia wake wa kutosafiri nchini Libya na kuahidi kuwasaidia wale ambao wako Libya ili waweze kurudi nchini mwao.

Taarifa hii ya mauaji ya Wakristo wa Ethiopia ni pigo kubwa kwa Ethiopia, moja ya taifa kongwe la Kikristo. Redwan Hussein amehakikisha kwamba kama Ethiopia haina kwa wakati huu nia ya kujiunga na muungano wa kijeshi dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu, Addis Ababa itaendelea kupambana dhidi ya Waislamu wenye itikadi kali za kidini kwenye mapigano mengine, kwa kuanzia kwa wanamgambo wa Al Shebab kutoka Somalia. Redwan Hussein amebaini kwamba tayari Ethiopia imewatuama wanajeshi wake nchini Somalia kujiunga na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika.