ETHIOPIA-IS-MAUJI-MAOMBOLEZO-USALAMA-HAKI

Siku tatu za maombolezo Ethiopia baada ya mauaji raia wake

Picha ya makao makuu ya Kanisa la Orthodox Addis Ababa, Ethiopia.
Picha ya makao makuu ya Kanisa la Orthodox Addis Ababa, Ethiopia. VBzi/Creative Commons

Baada ya kujizuia kuzungumza lolote Jumapili Aprili 19, serikali ya Ethiopia hatimaye imethibitisha Jumatatu wiki hii kwamba wanaume 30 waliouawa na kundi la Islamic State walikuwa Waethiopia waliotekwa nyara nchini Libya.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Afrika, wenye makao yake mjini Addis Ababa, Ethiopia, kupitia mwenyekiti wa Tume ya Umoja huo Nkosazana Dlamini-Zuma umelani kitendo hicho ulichokiita "ukatili na ujinga ". Wakati huohuo serikali ya Ethiopia imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, ambayo pia ni yanakwenda sambamba na kuwakumbuka raia wa kigeni kutoka Afrika waliouawa siku za hivi karibuni nchini Afrika Kusini kufuatia uhasama wa kibaguzi unaoendelea kushuhudiwa nchini humo.

Kuanzia Jumanne wiki hii maombolezo ya kitaifa yatashuhudiwa nchi nzima kwa siku tatu mfululuizo. Bunge linatazamiwa kutangaza rasmi leo Jumanne asubuhii, kabla ya kufanya tathmini ya uamzi unaoweza kuchukuliwa na nchi hiyo kama jibu kwa mauaji hayo. Bendera zitapeperushwa nusu mlingoti. Taasi za umma zitaendelea kufanya kazi.

Mauaji haya ya Wakristo wa Ethiopia ni pigo kubwa kwa Ethiopia, moja ya taifa kongwe la Kikristo. Awalli msemaji wa serikali ya Ethiopia Redwan Hussein alihakikisha kwamba kama Ethiopia haina kwa wakati huu nia ya kujiunga na muungano wa kijeshi dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu, Addis Ababa itaendelea kupambana dhidi ya Waislamu wenye itikadi kali za kidini kwenye mapigano mengine, kwa kuanzia kwa wanamgambo wa Al Shebab kutoka Somalia.

Redwan Hussein alibaini kwamba tayari Ethiopia imewatuama wanajeshi wake nchini Somalia kujiunga na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika.