AFRIKA KUSINI-UBAGUZI-USALAMA

Afrika Kusini: jeshi latumwa kuimarisha usalama

Timu ya maafisa wa usafi ya Manispaa ya Durban baada ya vijana wa Afika kusini kupora doka moja la mfanyabishara kutoka Somalia, Durban, Aprili 10 mwaka 2015.
Timu ya maafisa wa usafi ya Manispaa ya Durban baada ya vijana wa Afika kusini kupora doka moja la mfanyabishara kutoka Somalia, Durban, Aprili 10 mwaka 2015. AFP/RAJESH JANTILAL

Waziri wa ulinzi wa Afrika kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula, ametangaza Jumanne Aprili 21 kwamba jeshi litatumwa kuimarisha usalama katika vitongoji vya mji wa Alexandra, katika mkoa wa Johannesburg.

Matangazo ya kibiashara

" Jeshi llitatumia kama njia ya kuzuia uhalifu ambao umeendelea kushuhudiwa katika mji wa Alexandra ", amesema Nosiviwe Mapisa-Nqakula. Kwa wiki tatu, mashambulizi dhidi ya wageni yameendelea kuongezeka nchini Afrika Kusini. Mashambulizi hayo yalianza katika mji wa Durban, na katika siku za hivi karibuni yamesambaa katika mkoa wa Johannesburg.

Jeshi litatumwa kusaidia polisi, hasa katika mji wa Durban, katika mkoa wa Kwazulu Natal ambapo vurugu zilianza wiki tatu zilizopita, lakini pia katika kitongoji cha Alexandra katika mkoa wa Johannesburg, ambapo hali ya wasiwasi iliongezeka mara dufu tangu siku chache zilizopita.

Jumamosi iliyopita, raia wa Msumbiji alichomwa kisu mchana kweupe, na baadae alifariki. Picha ya mashambulizi hayo, iliyopigwa na mwandishi wa habari, ilirushwa hewani mara kadhaa na vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii. Tukio kilo liliibua hisia tofauti ndani na je ya Afrika Kusini. Jumatatu usiku wiki hii, raia wawili wa Wazimbabwe walijeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa risasi walipovamiwa nyumbani kwao katika mji wa Alexandra.

Waziri wa ulinzi anataka hali hiiyo ikomeshwe mara moja. Kwa mujibu wa Nosiviwe Mapisa-Nqakula, jeshi litakuwepo katika maeneo hayo ili kudumisha amani na kusaidia polisi ili kudhibiti ghasia.

Serikali ya Afrika Kusini ina wasiwasi kwamba huenda hali hiyo ikaongezeka iwapo hatua kali hazitochukuliwa, kwani mwaka 2008 raia wa kigeni 60 waliuawa katika ghasia dhidi ya wageni zilizotokea katika kitongoji kimoja cha mji wa Alexandra.