CAR-DRC-DIPLOMASIA-SHERIA

Romaric Vomitiadé atoroka, lakini akamatwa DRC

Waziri wa zamani wa utalii wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini, Romaric Vomitiadé amekamatwa katika kijiji cha Zongo, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya kupenya na kuvuka mpaka.

Waziri wa zamani hatiani kwa kosa la kubaka, Romaric Vomitiadé, alikamatwa katika kijiji cha Zongo, RDC.
Waziri wa zamani hatiani kwa kosa la kubaka, Romaric Vomitiadé, alikamatwa katika kijiji cha Zongo, RDC. RFI / Léa-Lisa Westerhoff
Matangazo ya kibiashara

Romaric Vomitiadé alikamatwa upande wa pili wa mto Oubangui katika mazingira ya ajabu.

Romaric Vomitiadé, kwa sasa amewekwa chini ya ulinzi, akituhumiwa kuingia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kinyume cha sheria. Waziri huyo wa zamani wa utalii wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Aprili 8 mwaka 2015 kwa kosa la kumbaka msichana mdogo.

Romaric Vomitiadé alizuiliwa jela katika jela za kitengo cha uchunguzi cha polisi lakini baadae aliachiliwa huru. Kutoroka nchi kwa waziri huyo wa zamani wa utalii wa Jamhuri ya Afrika kati kulitaka kuhatarisha uhusiano wa kidiplomasia ya Kinshasa na Bangui.

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ilipata taarifa kwamba Romaric Vomitiadé, alikimbilia katika kijiji cha Zongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Maafisa wa polisi wa Jamhuri ya afrika ya Kati walienda kumtafuta na kuingi katika ardhi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kinyume cha sheria za kimataifa. Hata hivyo maafisa hao walizuiliwa na polisi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Romaric Vomitiadé alisafirishwa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa na wakati huu amewekwa chini ulinzi. Wizara ya sheria ya Congo imesema inasubiri ombi rasmi la serikali ya Jamhuri ya Afrika la kutumwa Romaric Vomitiadé mjini Bangui. Hata hivyo wizara ya sheia ya Congo imesema itathmini ombi hilo.