Taarifa maalumu kuhusu uchaguzi Burundi

Nchini Burundi, Imbonerakure wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo mbalimbali vya ukatili dhidi ya raia.
Imehaririwa: 02/11/2020 - 17:11

Wakati mchakato wa uchaguzi ukiendelea nchini Burundi, hali ya wasiwasi imeendelea kutanda, huku joto la kisiasa likizidi kupanda kufuatia muhula watatu wa rais Pierre Nkurunziza. Zaidi ya watu 10,000 wameitoroka nchi hiyo kwa kuhofia kutokea machafuko baada ya kutangazwa jina la Pierre Nkurunziza kama mgombea wa chama tawala cha Cndd-Fdd. Katiba ya nchi ya Burundi na mkataba wa amani wa Arusha, ambao ni sheria mama ya nchi hiyo, vinapinga rais yoyote wa nchi hiyo kugombea zaidi ya miaka 10.