NIGER-BOKO HARAM-MAPIGANO-USALAMA

Niger yapoteza zaidi ya wanajeshi 50

Wanajeshi wa Niger wakipiga doria kwenye eneo la mpaka na Nigeria.
Wanajeshi wa Niger wakipiga doria kwenye eneo la mpaka na Nigeria. RFI/Nicolas Champeaux

Zaidi ya wanajeshi hamsini wa Niger wanasadikiwa kuawa katika shambulio lililoendeshwa na kundi la kiislamu la Boko Haram Jumamosi mwishoni mwa juma hili lililopita.

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao walikua wakipiga kambi katika kisiwa cha Karamga, katika ziwa Chad. Wizara ya Ulinzi ya Niger haijathibitisha idadi hiyo ya vifo vya wanajeshi wake, lakini imebaini katika tangazo ililotoa kwamba “ operasheni zinaendelea” kwa kuwaondoa wanamgambo wa Boko Haram katika kisiwa hicho.

Kundi la kiislamu la Boko Haram ililiendesha shambulio mapema Jumamosi asubuhi dhidi ya wanajeshi 120 waliokua wakipiga kambi katika kisiwa cha Karamga, kwenye mwambao wa ziwa Chad. Wanajeshi wa Niger waliamua kutimka baada ya kuzidiwa nguvu. Inaarifiwa kuwa shambulio hilo liliendesha na zaidi ya wapiganaji 2000 wa Boko Haram, ambao walikua na zana nzito za kijeshi. Kwa sasa kisiwa hicho cha Karamga kinashikiliwa na Boko Haram.

Kwa mujibu wa mashahidi katika mji wa Diffa, mji mkuu wa jimbo la kusini mashariki mwa Nigeria, mapigano hayo yaligharimu maisha ya wanajeshi 48 wa Niger na wengine 36 hawajulikani walipo. Itakua ni pigo kubwa kwa serikali ya Niger iwapo taarifa hii itathibitishwa. Hata hivyo taarifa ya mapigano imethibitishwa katika tangazo la wizara ya ulinzi, lakini hakuna idadi ya hasara iliyotolewa.

Kwa upande wake rais Mahamadou Issoufu, ameitisha kikao cha dharura cha baraza la usalama la kitaifa, linaloundwa na viongozi wa jeshi na viongozi wa taasisi mbalimbli za nchi. Rais wa Niger amewataka wanajeshi kutumwa katika kisiwa cha Karamga ili kuwafurusha wapiganaji wa Boko Haram.