NIGERIA- AFRIKA kUSINI-DIPLOMASIA

Nigeria yamrudisha nyumbani balozi wake

Afrika Kusini imelaani hatua ya Nigeria kumrudisha nyumbani Balozi wake kutokana na uvamizi unaoendelea dhidi ya wageni nchini mwao.

Wahamiaji wakikimbilia katika kambi ya Primrose nje ya mji wa Johannesburg, Aprili 18 mwaka 2015, ili kuepuka mateso na unyanyasaji dhidi ya wageni vinavyoshuhudiwa Afrika Kusini.
Wahamiaji wakikimbilia katika kambi ya Primrose nje ya mji wa Johannesburg, Aprili 18 mwaka 2015, ili kuepuka mateso na unyanyasaji dhidi ya wageni vinavyoshuhudiwa Afrika Kusini. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Nigeria inasema kuwa ilichukua hatua hiyo kutokana na raia wake kuvamiwa na mali zao kuharibiwa na wananchi wa Afrika Kusini.

Tangu kuzuka ghasia dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini mwezi mmoja uliopita, watu saba wameuawa na wengine kukimbilia katika kambi za wakimbizi.

Mfalme wa jamii ya Zulu Goodwill Zwelithini amekuwa akilaumiwa kwa kuchochea uvamizi huo kwa matamshi aliyotoa kuwa wageni warudi kwao.

Hata hivyo, Mfalme huyo amewataka wananchi kuacha uvamizi huo huku akivilaumu vyombo vya habari kwa kumnukuu viibaya.

Wabunge nchini humo kuanzia leo Jumatatu hawatakuwa bungeni ili kwenda katika maeneo yao na kuwahimiza wananchi kuacha kuwavamia wageni.