DRC-UPINZANI-CENI-SIASA

DRC : upinzani walaumu

Upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo umeelezea masikitiko yake kufwatia kushindwa kukutana na mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi, nchini humo Ceni, padre Appolinaire Malu Malu.

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi Ceni Appolinaire Malu Malu,
Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi Ceni Appolinaire Malu Malu, (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa viongozi wa vyama hivyo vya upinzani unasema uliomba kukutana na mwenyekiti huyo wa Ceni jana Jumatatu, mjini Kinshasa ambapo walitamani kutoa mapendekezo yao kuhusu kalenda ya uchaguzi unaopangwa kufanyika nchini humo.

Upinzani unasema una wasiwasi kutokana na kuwa mapendekezo yao hayo hayakuwasilishwa moja kwa moja kwa muhusika.

Viongozi hao wa upinzani walipokelewa na naibu mwenyekiti wa Ceni, Andre Pungwe kutoka chama tawala cha PPRD, huku wakielezea kuwa tangu kuonekana kwa Malu Malu Aprili 16, hajaonekana kwa mara nyingine tena kuwasilikiza.