NIGER-BOKO HARAM-MAUAJI-USALAMA

Jeshi lathibitisha kuuawa kwa mamia ya watu Damasak

Mamia ya watu wamekutwa wameuawa katika mji wa Damasak, kaskazini mwa Nigeria mwanzoni mwa juma hili, maafisa wakuu wa jeshi la serikali ya nchi hiyo wamethibitisha.

Bendera iliyopokonywa kutoka mikononi mwa vikosi vya Boko Haram, ikishikiliwa na wanajeshi wa Niger, ambao wameingia katika mji wa Damasak, nchini Nigeria, Machi 18 mwaka 2015.
Bendera iliyopokonywa kutoka mikononi mwa vikosi vya Boko Haram, ikishikiliwa na wanajeshi wa Niger, ambao wameingia katika mji wa Damasak, nchini Nigeria, Machi 18 mwaka 2015. REUTERS/Emmanuel Braun
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mashirika ya kimisaada, wapiganaji wa Boko Haram waliokuwa na bunduki waliwaua kwa risasi na kuwachoma moto maelfu ya raia waliokuwa wakijaribu kukimbia kunusuru maisha yao kupitia ziwa Chad, baada ya wapiganaji hao kuwazidi nguvu wanajeshi wa serikali mwishoni mwa juma lililopita.

Jeshi na maofisa wa Serikali wa Niger awali walithibitisha kambi yao kuvamiwa na wapiganaiji wa Boko Haram April 25 bila ya kusema ni wanajeshi wangapi wa Nigeria walipoteza maisha.

Kwa mujibu wa mashahidi katika mji wa Diffa, mji mkuu wa jimbo la kusini mashariki mwa Nigeria, mapigano hayo yaligharimu maisha ya wanajeshi 48 wa Niger na wengine 36 hawajulikani walipo. ara ya ulinzi, lakini hakuna idadi ya hasara iliyotolewa.

Kundi la kiislamu la Boko Haram ililiendesha shambulio mapema Jumamosi asubuhi dhidi ya wanajeshi 120 waliokua wakipiga kambi katika kisiwa cha Karamga, kwenye mwambao wa ziwa Chad. Wanajeshi wa Niger waliamua kutimka baada ya kuzidiwa nguvu. Inaarifiwa kuwa shambulio hilo liliendesha na zaidi ya wapiganaji 2000 wa Boko Haram, ambao walikua na zana nzito za kijeshi. Kwa sasa kisiwa hicho cha Karamga kinashikiliwa na Boko Haram.