TOGO-UCHAGUZI-SIASA

Togo: Faure Gnassingbé atangazwa mshindi

Rais Faure Gnassingbé katika mkutano wa hadhara mjini Tado, Togo, Aprili 13 mwaka 2015.
Rais Faure Gnassingbé katika mkutano wa hadhara mjini Tado, Togo, Aprili 13 mwaka 2015. REUTERS/Noel Tadegnon

Tume ya uchaguzi nchini Togo imemtangaza Faure Gnassingbé, kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita, kwa kujikusanyia asili mia 58.75 ya kura wakati mpinzani wake mkuu Jean-Pierre Fabre asilimia 34.95.

Matangazo ya kibiashara

Tume ya Kitaifa ya uchaguzi inasema kufwatia uthibitisho wa Mahakama ya Katiba matokeo ya muda yameonyesha kuwa Faure Essozimna Gnassingbé, amechaguliwa kuliongoza taifa hilo kwa muhula wa tatu, alisema Taffa Tabiou , msemaji wa tume ya uchaguzi nchini Togo.

Faure Gnassingbé amekuwa madarakani tangu babake Gnassingbé Eyadema, aage dunia baada ya kuchukua mamlaka mwaka 1967.

Faure Gnassingbé yuko madarakani kwa kipindi cha miaka 10 tangu mwaka 2005 baada ya kifo cha babake

Hata hivyo hivyo matokeo hayo ni ya muda, hadi pale yatasahihishwa na Korti ya Katiba. Itafahamika kwamba rais huyo alimshinda mshindani wake Jean-Pierre Fabre kwa asilimia ndogo ikilinganishwa na mwaka 2015, ambapo alipata zaidi ya asilimia 60.