CAR-UFARANSA-UBAKAJI-HAKI

CAR: wanajeshi wa Ufaransa watuhumiwa kuwanajisi watoto

Serikali ya Ufaransa imetangaza kuanzisha uchunguzi kufwatia tuhuma zinazowakabili wanajeshi wake wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya kati kutekeleza vitendo vya unyanyasaji wa kimapenzi dhidi ya watoto.

Unyanyasaji wa kijinsia unadaiwa kufanywa kati ya mwezi Desemba mwaka 2013 na mwezi Mei mwaka 2014. Wanajeshi 16 wa Ufaransa wanatuhumiwa kuhusika na vitendo hivyo.
Unyanyasaji wa kijinsia unadaiwa kufanywa kati ya mwezi Desemba mwaka 2013 na mwezi Mei mwaka 2014. Wanajeshi 16 wa Ufaransa wanatuhumiwa kuhusika na vitendo hivyo. AFP PHOTO / ERIC FEFERBERG
Matangazo ya kibiashara

Nakala ya Ripoti inayobaini vitendo hivyo imewakilishwa kwenye gazeti la The Guardian la Uingereza na shirika lisilo la kiserikali “Aids Free World” ambapo wizara ya sheria ya Ufaransa imekiri tayari kuanza uchunguzi unaosimamiwa na Mwendesha mashtaka wa mjini Paris.

Akihojiwa na RFI, mkurugenzi wa shirika hilo, Paula Donovan, amesema wamefanya mahojiano na wasichana wadogo sita ambao walifanyiwa kitendo hicho cha udhalilishaji wa kingono na kubaini kuwa walifanyiwa kitendo hicho zaidi ya wasichana 20 wenye umri kati ya miaka minane na kumi na mbili.

Inaarifiwa kuwa zaidi ya wanajeshi kumi na tano wa Ufaransa walihusika katika kitendo hicho.

Vitendo hivyo vya aibu vilitekelezwa katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Mpoko, karibu na uwanja wa ndege wa Bangui, walikokua wakipiga kambi wanajeshi wa Ufaransa, kati ya mwezi Desemba mwaka 2013 na Mei mwaka 2014. Mahojiano na wasichana hao yalifanyika kati ya mwezi wa Mei na Juni mwaka 2014.

Viongozi wa Ufaransa walifahamishwa hali hiyo. Wizara ya sheria imethibitisha kwamba uchunguzi wa mwazo ulianzishwa mwezi Julai mwaka 2014.

Wakati hayo yakijiri, jukwaa la vyama vya siasa la msaada kwa serikali ya mpito AFDT, linapinga ushiriki wa marais wa zamani Francois Bozizé na Michel Djotodia katika kongamano la kitaifa linalotarajiwa kwa vile viongozi hao wamechangia kuiweka nchi hiyo katika hali isio sawa kama anavyobainisha Nicolas Tiangaye Mwenyekiti wa Jukwaa hilo.