DRC-JAMII-USALAMA-HAKI

DRC: wanaharakati wanne wa Lucha waachiliwa huru

Mmoja kati ya waandamanaji akamatwa na polisi Goma, Mashariki mwa DRC, Januari 19 mwaka.2015.
Mmoja kati ya waandamanaji akamatwa na polisi Goma, Mashariki mwa DRC, Januari 19 mwaka.2015. REUTERS/Kenny Katombe

Wanaharakati wanne kutoka taasisi ya vijana wanaotetea demokrasia na utawala bora, Lucha waliokuwa wanashikiliwa mjini Goma, mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, wameachiwa huru kwa dhamana.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa gereza la Munzenze walikokuwa wamezuiliwa vijana hao, Joseph Mirindi, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa wanaharakati hao waliachiwa huru majira ya alasiri jana jumatano Aprili 29.

Taasisi hiyo imesema walioachiwa huru kwa dhamana ni pamoja na Vincent Kasereka, Trésor Akili, Sylvain Mumbere na Gentil Mulume.

Watu ho wameachiliwa kwa dhamana ya dola za kimarekani zaidi ya Mia tano.

Hata hivyo taasisi ya vijana wanaotetea demokrasia na utawala bora, Lucha, inasema mwanahaarakati wao Fred Bauma aliyekamatwa na wengine zaidi ya kumi mjini Kinshasa mnamo machi 15, mwaka huu, anaendelea kushikiliwa katika Idara ya ujasusi, ANR, na kwamba haruhusiwi kukutana na wakili wake, wala watu wa familia yake.