NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Zoezi la kuwatambua wanawake na wasichana 300 laanza

Serikali ya nigeria inasema imeanza kuwatambua zaidi ya wanawake na wasichana 300 waliokolewa mikononi mwa kundi la kigaidi la Boko Haram mwanzoni mwa juma hili.

Maandamano ya kuishinikiza serikali kufanya kikilyochini ya uwezo wake ili kukomboa wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na Boko Harammwaka mmoja uliyopita.
Maandamano ya kuishinikiza serikali kufanya kikilyochini ya uwezo wake ili kukomboa wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na Boko Harammwaka mmoja uliyopita. Reuters/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imeleta matumaini kwa wazazi ambao wasichanaa wao walitekwa na Boko Haram wakiwa shuleni katika eneo la Chibok mwaka uliopita.

Hata hivyo jeshi la Nigeria limesema halina uhakika kuwa wasichana waliokolewa ni wale wa Chibok.

Awali msemaji wa Jeshi hilo Sani Oussmane, alisema watoto hao wa kike waliookolewa si miongoni mwa wale waliotekwa mwaka mmoja uliopita na kundi la kiislamu katika eneo la Chibok.

Sani Ousmane alisema kwamba wanawake na watoto hao wa kike walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo silaha pia zilikamatwa, baada ya kuziharibu kambi hizo.

Katika tangazo liliyorushwa hewani kwenye mtandao wa Twitter Jumanne Jioni, jeshi la Nigeria lilitangaza kwamba limewaokoa angalau wasichana 200 na wanawake 93. Kuokolewa kwa watu hao kunakwenda sambamba na operesheni ya jeshi dhidi ya makambi ya Boko Haram katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.