DRC-MONUSCO-ADF-USALAMA

DRC: Monusco yawapoteza wanajeshi wake wawili

Kikosi cha Umoja wa Mataifa, Monusco kikipiga doria Kivu-Kaskazini, Aprili 10 mwaka 2010.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa, Monusco kikipiga doria Kivu-Kaskazini, Aprili 10 mwaka 2010. Photo MONUSCO/Abel Kavanagh

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ndani ya massa 24, baaada ya shambulio dhidi ya helikopta ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ncghini humo, Monusco, msafara wa magari ya Ujumbe huo umeshambulia Jumanne usiku Mei 5 katika eneo hilo kuliko shambuliwa helikopta hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Watu wanaosadikiwa kuwa waasi wa Uganda wa ADF wananyooshewa kidole kuhusika katika shambulio. Kundi la waasi la ADF linaendesha harakati zake katika eneo hilo tangu zaidi ya miaka 20 iliyopita. Mpaka sasa wanajeshi wawali wa Monusco ndio wanaripotiwa kuuawa na wengine wengi wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na mmoja ambaye yuko katika hali ya maututi.

Shambulio hilo dhidi ya msafara wa magari ya Monusco limeendeshwa saa moja na nusu usiku. Zaidi ya wanajeshi ishirini wa Monusco kutoka Tanzania wamekua wakipiga doria kwenye barabara kuu inayotokea Beni kuelekea Mayimoya, karibu na kambi ya jeshi ya Mavivi, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Shambulio hilo lilitokea kilomita zaidi ya kumi kusini mwa mji wa Eringeti.

Hakuna taarifa zaidi kuhusu shambulio hilo, lakini wanajeshi wawili ndio wameuawa na wengine kumi wamejeruhiwa. Jumanne usiku wiki hii, wanajeshi watano kutoka Tanzania wamekosekana katika kambi hiyo ya kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi hao wa kikosi cha Umoja wa Mataifa wamekua wakipiga doria peke yao, kwani tangu mwezi Mach jeshi la Congo (FARDC) lilisitisha operesheni na zoezi la kupiga doria, ambazo jeshi hilo lilikua likiendesha na kikosi cha Umoja wa Mataifa, Monusco, katika mkoa mzima wa Kivu-Kaskazini. Jumanne usiku wiki hii, baada ya kupata taarifa ya shambulio hilo, jeshi la Congo liliwatuma wanajeshi wake wengi kwenye eneo la tukio.

Shambulio hilo linatokea ndani ya masaa 24 baada ya helikopta ya Monusco kushambuliwa. Mpaka sasa hakuana kundi lolote ambalo limkiri kuhusika na mashambulizi hayo. Umoja wa Mataifa unshuku kuwa mashambulizi hayo yametekelezwa na waasi wa Uganda wa ADF.

Katika mtandao wa kijamii wa Twitter, mkuu wa Monusco Martin Kobler ameelezea maskitiko yake na kusikitishwa na mashambulizi hayo.