Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-Mapigano-Usalama-SIASA

Mapigano yaendelea kurindima Sudani Kusini

Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. Lakini, rais wa Sudani Kusini  na mpinzani wake, hawakusiriki katika mazungumzo ya amani, Addis Ababa, Ethiopia.
Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. Lakini, rais wa Sudani Kusini na mpinzani wake, hawakusiriki katika mazungumzo ya amani, Addis Ababa, Ethiopia. REUTERS/Goran Tomasevic
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Jeshi la Sudan Kusini limesema linafanikiwa kuchukua ngome kadhaa za waasi. Msemaji wa jeshi Philip Aguer amesema mji wa Bentiu na Leer inaelekea kuwa mikononi mwa wanajeshi wa serikali.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa umeendelea kulalamikia kudorora kwa hali ya usalama katika majimbo ya unity na Upper Nile wakati huu wafanyakazi wa Mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yakiondoka katika majimbo ambayo vita vinaendelea.

Mazungumzo ya amani ya kupata suluhu nchini Sudan Kusini yameshindikana.

Hali ya Sudan Kusini imechukua mkondo mpya kwani kumezuka kikundi kipya cha waasi wanaoongozwa na  Meja jenerali maarufu aliyetoroka kutoka jeshi la serikali.

Tayari Meja Jenerali huyo Johnson Olony, ametungua helikopta mbili za kijeshi zilizotumwa kushambulia ngome yake mpya  huko Malakal, mji mkuu wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Upper Nile.

Siku moja baada ya serikali ya Sudan Kusini kutangaza kuwa vikosi vyake vimeudhibiti mji wa Malakal, ulioko Kaskazini mwa mji mkuu Juba, mambo yamebadilika, kwani  mapigano makali yamezuka kati ya waasi wa kundi jipya la waasi na majeshi ya Sudan Kusini katika Malakal, mji mkuu wa jimbo la Upper Nile.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.