MALI-MAZUNGUMZO-USALAMA

Serikali ya Mali na makundi yenye silaha wakutana Algeria

Waziri wa mambo ya nje wa Mali, Abdoulaye Diop, wakati wa kutia saini kwenye mkataba wa amani, Bamako,Mei 15 mwaka 2015.
Waziri wa mambo ya nje wa Mali, Abdoulaye Diop, wakati wa kutia saini kwenye mkataba wa amani, Bamako,Mei 15 mwaka 2015. AFP PHOTO / HABIBOU KOUYATE

Mkutano mpya kati ya serikali ya Mali na makundi yenye silaha ya kaskazini mwa Mali yanatazamiwa kuanza leo Jumatatu nchini Algeria, kwa mujibu wa jumuiya ya kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Wawakilishi wa muungano wa makundi yenye silaha Azawad (MCA) yanatazamiwa kuwasili nchini Algeria leo Jumatatu jioni. Hata kama muungano huo ulisahihisha mkataba wa amani, haukuwepo katika sherehe za kutia saini mkataba huo katika mji mkuu wa Mali, Bamako.

Makundi hayo ndiyo yaliyoomba kukutana kwa mazungumzo na viongozi wa Mali kabla ya kuomba kutia saini kwenye mkataba wa amani.

Bilal Ag Chérif, katibu mkuu wa muungano wa makundi yenye silaha kaskazini mwa Mali( CMA), wakati wa kusahihisha mkataba wa amani, Alhamisi Mei 14, Algiers.
Bilal Ag Chérif, katibu mkuu wa muungano wa makundi yenye silaha kaskazini mwa Mali( CMA), wakati wa kusahihisha mkataba wa amani, Alhamisi Mei 14, Algiers. REUTERS/Zohra Bensemra

Lengo la mkutano huu pia ni kutafuta ufumbuzi kwa kuimarisha usitishwaji vita, wakati ambapo mapigano yameendelea kushuhudiwa kaskazini mwa Mali.

Mdororo wa usalama na mapigano vimeendelea kushuhudiwa kati ya pande hasimu katika jimbo la Tombouctou, kaskazini madharibi.Hali hiyo imesababisha raia wengi kuyahama makaazi yao.