UN-JUBA-DIPLOMASIA

UN yalaani uamzi wa serikali ya Juba

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, katika makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa nchini Ethiopia, Oktoba 28 mwaka 2014.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, katika makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa nchini Ethiopia, Oktoba 28 mwaka 2014. AFP PHOTO / Zacharias Abubeker

Umoja wa Mataifa umelaani hatua ya serikali ya Sudan Kusini kumfukuza nchini humo mwakilishi wake anayeshughulikia maswala ya kibinadamu, Toby Lanzer.

Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki Moon ameitaka serikali ya Juba kubadilisha uamuzi huo haraka iwezekanavyo ili raia wanaokimbia kutokana na machafuko waendelea kupata msaada wake.

Bwana Lanzer, raia wa Uingereza amesema hakupewa sababu yoyote ya kutakiwa kuondoka nchini humo.

Hata hivyo, muda wa kuhudumu kwa Lanzer ulikuwa unafikia ukingoni na nafasi hiyo itachukuliwa na Eugene Owusu kutoka Ghana.

Wakati huo huo viongozi wa Afrika Mashariki wamerejelea tena jitihada za kuwapatanisha viongozi wa Sudan Kusini, rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar ili kumaliza mzozo unaondelea.

Ujumbe wa wawakilishi kutoka mataifa hayo pamoja na wanasiasa wa upinzani watano akiwemo katibu mkuu wa chama cha SPLM, Pagan Amum, waliokamatwa na kuachiliwa huru na serikali ya Juba na kwenda kuishi nchini Kenya walirudi nyumbani Jumatatu wiki hii.

Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ndiye aliongoza ujumbe wa kuwarejesha wanasiasa hao nyumbani.