MALI-USALAMA

Mdororo wa usalama waendelea kushuhudiwa Mali

Rais wa MaliIbrahim Boubacar Keïta, Septemba 9 mwaka 2013.
Rais wa MaliIbrahim Boubacar Keïta, Septemba 9 mwaka 2013. AFP PHOTO / HABIBOU KOUYATE

Watu 3 wamepoteza maisha katika shambulio la watu waliokuwa na silaha kaskazini mwa Mali, duru za usalama zimethibitisha na kushindwa kubaini iwapo ni tukio la kijambazi au la makundi ya waasi.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo linajiri wakati huu kundi la waasi wa Kitwareg ambalo limekuwa likijadiliana huko Alger nchini Algeria, linaelekea kutia saini hii leo Ijumaa makubaliano ya usalama yatayofikia kwenye usitishwaji wa mapigano katika eneo la kaskazini mwa Mali.

Hakuna duru yoyote iliyothibitisha iwapo mauaji hayo ya watu watatu yana uhusiano wowote na makundi ya waasi au ni ujambazi, lakini duru kutoka kundi la waasi wa Kitwareg limesema mmoja kati ya waliouawa ni mfuasi wa kundi hilo na kulituhumu kundi la waasi wanaunga mkono serikali kwamba ndio waliohusika

Mbali na hayo, raia mmoja alipigwa risase hivi majuzi karibu na kitongoji cha Goundam karibu na mji wa Timbuktu na watu waliokuwa na silaha ambao walikuwa kwenye gari, taarifa ambayo ilithibitishwa na duru za usalama wa nje ya taifa hilo ziliyofahamisha pia mauaji ya raia mwingine katika mji wa Timbuktu

Katika hatuwa nyingine, mtu mmoja alietekwa mjini Menaka mwanzoni mwa juma hili na kundi la watu waliokuwa na silaha amekutwa amekufa kaskazini mashariki mwa Mali karibu na mpaka na Niger.