MALI-JIHADI-USALAMA

Shambulio la kwanza la wanajihadi kusini mwa Mali

Kwa kawaida wanajihadi wamekua wakiendesha harakati zao katika eneo la kaskazini mwa Mali, hasa katika jimbo laTimbuktu, ambapo vikosi vya Ufaransa na Mali vinashirikiana, kama hapa wakati wa operesheni "Madine 3".
Kwa kawaida wanajihadi wamekua wakiendesha harakati zao katika eneo la kaskazini mwa Mali, hasa katika jimbo laTimbuktu, ambapo vikosi vya Ufaransa na Mali vinashirikiana, kama hapa wakati wa operesheni "Madine 3". AFP PHOTO / PHILIPPE DESMAZES

Askari polisi mmoja ameuawa na watu wawili wamejeruhiwa katika shambulio lililoendeshwa na Jumatano Asubuhi wiki hii dhidi ya kijiji kimoja kusini mwa Mali.

Matangazo ya kibiashara

Magari na pikipiki vilichomwa katika shambulio hilo. Wanajihadi wananyooshewa kidole kuhusika na shambulio hilo, kwani inasemekana kuwa walipandisha bendera yao katika kambi moja ya kijeshi katika moja ya eneo la kusini mwa Mali kabla ya kutoweka.

Kumeripotiwa mapigano makali kati ya jeshi la Mali na wapiganaji wa kijihadi katika mji huo wa Sikasso, Maafisa wakuu wa Jeshi la nchi hiyo Wamethibitisha,

Ni kwa mara ya kwanza wanajihadi wanahusishwa katika shambulio lililoendeshwa katika jimbo la Sikasso linalopakana na Côte d’Ivoire na Burkina-Faso. Haijafahamika iwapo wauaji hao walitokea nchini Côte d’Ivoire.

Msemaji wa jeshi la polisi nchini Mali amesema hii ni mara ya kwanza kufanyika kwa mapigano ya kijihadi katika eneo hilo, huku akiongeza kuwa polisi aliyekuwa akipiga doria katika eneo hilo, alipoteza maisha wakati wa majibizano ya risasi, na kwamba watu wawili, raia wa kawaida walijeruhiwa.

Baadhi ya wawakilishi wamebaini kwamba bado kuna makundi ya wanajihadi kusini mwa Mali mbayo hayajajitangaza kuanzisha harakati zao, aidha ni kundi la wanajihadi waliotokea nchini Côte d’Ivoire, na kuingia Mali.