CHAD-MASHAMBULIZI-USALAMA

Chad: Ndjamena yawekwa chini ya ulinzi mkali baada ya mashambulizi

takribani watu 27 waliuawa katika mfululizo wa mashambulizi ya kujitoa mhanga yaliyotokea  Ndjamena Juni 15 mwaka 2015.
takribani watu 27 waliuawa katika mfululizo wa mashambulizi ya kujitoa mhanga yaliyotokea Ndjamena Juni 15 mwaka 2015. REUTERS/Moumine Ngarmbassa

Siku mbili baada ya mji mkuu wa Chad, Ndjamena kukumbwa na mfululizo wa mabomu na kusababisha vifo vya watu 27, na zaidi ya mia moja kujeruhiwa, hatua za kiusalama zimeimarishwa katika mji huo na operesheni ya kuwakamata wahusika imeanza.

Matangazo ya kibiashara

" Mashambulizi haya hayatopotosha dhamira ya Chad ya kupambana dhidi ya ugaidi ", imeahidi serikali ya Chad, ambayo imeonyesha msimamo wake sawa na ule wa Idriss Deby Jumanne aliporejea nchini mwake baada ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mjini Johannesburg.

Usalama umeimarishwa katika mji wa Ndjamena. Mji ambao umezingirwa na vikosi vya usalama. Askari polisi na wanajeshi wamepelekwa kwa wingi karibu na misikiti, makanisa, masoko na katika maeneoambako kunakusanyika watu wengi. Magari na nyumba vimekua vikifanyiwa msako. Magari yenye vioo visiyoonyesha yamepigwa marufuku. Barabara zinazoingia Ikulu na kituo kikuu cha polisi zimezuliliwa.

Idriss Deby amesema waliotekeleza kitendo hiki wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Rais huyo wa Chad amesikitika kuwa pamoja na kupitia upya maelekezo yake kwa serikali, umakini dhidi ya hatari ya mashambulizi ulikua imarakwa kiasi fulani. Idriss Deby pia ametoa rambirambi zake kwa familia za wahanga. Kwa upande wake rais wa Chad, amesema hakuna shaka kuwa mashambulizi hayo yalitekelezwa kutokana na pigo kubwa walilolipata wanamgambo wa Boko Haram.

Wakati huo huo, uchunguzi umeanzishwa. Mwendesha mashitaka katika mji wa Ndjamena ameanzisha uchunguzi. Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka, watuhumiwa kadhaa wamekamatwa. Wadhamini na na wahusika wengine wanatafutwa, kwani operesheni kama hiyo inahitajika maandalizi makubwa, amesema mwendesha mshtaka wa mji katika mji wa Ndjamena.