ANGOLA-USALAMA

Angola : watu zaidi ya 10 wakamatwa

Vijana waliokamatwa wanaomba kuondoka kwa rais wa Angola, José Eduardo dos Santos, madarakani tangu mwaka 1979.
Vijana waliokamatwa wanaomba kuondoka kwa rais wa Angola, José Eduardo dos Santos, madarakani tangu mwaka 1979. © Getty Images/Sean Gallup

Polisi nchini Angola wamewakamata watu 13 ambao ni waharakati wa upinzani. Wanaharakati hao ni vijana na miongoni mwa waliokamatwa ni mwanamuziki Luaty Beirao.

Matangazo ya kibiashara

Polisi inawatuhumu vijana hawa kwamba walikua na lengo la kuvuruga usalama.

Hata hivyo makundi ya wanaharajati na yale ya kutetea haki za binadamu yanadai kuwa vijana waliokamatwa ni zaidi ya 20 baada ya polisi kuvamia mkutano wa vijana jijini Luanda.

Tangu mwaka 2011, vijana nchini Angola wamekuwa wakitaka kuondoka madarakani kwa rais José Eduardo dos Santos ambaye amekuwa rais kwa miaka 35 sasa.

José Eduardo dos Santos anataka kuepuka kabisa maandamano ya vijana ambayo yanaweza kuvutia vijana wengine na kusamba nchi nzima. Utaratibu huu unaotumiwa na polisi ya Angola unaonyesha kwamba unadhibiti hali ya mabo ynchini humo. Lakini pia utaratibu huu unaonyesha udhaifu fulani.