Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Kukamatwa kwa mkuu wa usalama wa taifa la Rwanda mjini London Uingereza, kutoroka nchi kwa spika wa bunge na naibu wa pili wa rais nchini Burundi

Sauti 21:41

Katika makala hii tunaangazia kukamatwa kwa mkuu wa usalama wa taifa la Rwanda Emmanuel Karenzi kareke mjini London Uingereza, ambaye baadaye aliachwa huru kwa dhamana, lakini pia maandamano ya mjini Kigali mbele ya ubalozi wa uingereza huku wananchi wakiishinikiza serikali ya uingereza kumwacha huru afisa huyo wa usalama.Pia tumeangazia hali ya wasiwasi nchini Burundi wakati nchi hii ianelekea kwenye uchaguzi mkuu wa urais julai 15 ukitangulizwa na ule wa wabunge jumatatu Juni 29 mwaka huu; na nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa juma tumeangazia malalamiko ya rais Joseph Kabila yaliyowasilishwa mbele ya mahakama moja mjini Kinshasa, akiwatuhumu baadhi ya amagavana kuhusika na ubadhirifu pia ufujaji wa mali ya umma.Kimataifa, tumeangazia tukio la kigaidi katika kampuni moja ya gesi mjini Isere nchini Ufaransa.Karibu tujumuike sote.