Pata taarifa kuu
MISRI-MAUAJi-USALAMA

Ngome za jeshi zashambuliwa Sinaï

Randabauti ya jeshi katika mji wa Arish, Kaskazini mwa Sinaï, Julai 15 mwaka 2013.
Randabauti ya jeshi katika mji wa Arish, Kaskazini mwa Sinaï, Julai 15 mwaka 2013. REUTERS/Stringer
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Nchini Misri, takriban wanajeshi na raia 38 wameuawa ikiwani pamoja na wanamgambo wa kiislamu 38, Kaskazini mwa eneo la Sinaï katika mfululizo wa mashambulizi, kwa mujibu wa jeshi la Misri.

Matangazo ya kibiashara

Ngome tano za jeshi zimeshambuliwa kwa wakati mmoja katika jimbo linalochukuliwa kama ngome kuu ya kundi la wanamgambo wa kiislamu wenye uhusiano na kundi la Islamic State. Shambulio hilo ni moja ya mashambulizi ambayo yamesababisha vifo dhidi ya wanajeshi wa Misri katika jimbo hilo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Cairo, Alexandre Buccianti, ngome tano za jeshi la Misri, ziliyo pembezoni mwa mji wa Cheikh Zoweid karibu na mpaka na Ukanda wa Gaza nchini Palestina, zimeshambuliwa kwa wakati mmoja na mamia ya wanamgambo wa kiislamu. Washambuliaji walikua katika magari madogo aina ya DW4. Walikua wamebebelea silaha za kurusha makombora, silaha za kivita na silaha za kudungua ndege.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, wanamgambo hao walitimka baada ya kutumwa kikosi cha wanajeshi wengine katika eneo hilo la Sinaï.

Helikopta za jeshi zimekua zikiwatafuta washambuliaji hao. Shambulio hilo limetokea baada ya miezi tisa ya kuripotiowa hali ya utulivu katika eneo la Sinaï, na siku moja baada ya maadhimisho ya pili ya maandamano dhidi ya rais wa zamani wa Misri kutoka kundi la Muslim Brotherhood, Mohamed Morsi. Watu kutoka Chechenia ni miongoni mwa wanajihadi hao walioendesha shambulio hilo, ambao waliahidi kuutii kundi la Islamic State.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.