MALI-UFARANSA-USALAMA

Mali: AG Wadoussène auawa

Mwanajeshi wa Ufaransa wa operesheni Barkhane, nchini Mali, Novemba 5 mwaka 2014.
Mwanajeshi wa Ufaransa wa operesheni Barkhane, nchini Mali, Novemba 5 mwaka 2014. .REUTERS/Joe Penney

Jeshi la Ufaransa limetangaza kumuua mmoja wa viongozi wanaosadikiwa kuhusika na mauaji ya waandishi wa habari wa RFI nchini Mali tarehe 2 mwezi Novemba mwaka 2013 mjini Kidal.

Matangazo ya kibiashara

Kuuawa kwa Mohamed Ali Ag Wadoussène ni pigo kubwa kwa tawi la wanajihadi la AQMI linalodaiwa kutekeleza utekaji nyara wa raia wa Ufaransa Serge Lazarevic.

Mohamed Ali Ag Wadoussène alikuwa anaongoza uhalifu uliopelekea mauaji ya waandishi wa habari wawili wa RFI, Ghislaine Dupont na Claude Verlon.

Makao makuu ya jeshi nchini Ufaransa yamethibitisha taarifa hiyo ya kuuawa kwa Wadoussène katika operesheni ya vikosi maalum kaskazini mwa Mali ambapo wanajihadi wawili wamekamatwa, huku askari wawili wa Ufaransa wakijeruhiwa katika operesheni hiyo.

Wadoussène alikuwa kiuongo muhimu katika itifaki ya wanajihadi hao ambaye kwa kipindi cha miaka kadhaa ameongeza kwa ushawishi mkubwa kaskazini mwa Mali chini ya Iyad AG Ghali, kiongozi mkuu wa Ansar Dine, kundi lenye ushirika wa karibu na AQMi.

Kuawa kwa Abdelkrim el-Targui katikati ya mwezi Mei kulivunja kichwa cha uongozi wa kiufundi wa wanajihadi hao na sasa operesheni Barkane ya Ufaransa dhidi yao katika ukanda wa Sahel inadhamiria kulisambaratisha kundi hilo la AQMI.