ICC-COTE D'IVOIRE-SHERIA

ICC yachunguza makosa yanayowakabili viongozi wa zamani wa waasi waliomuunga mkono Ouattara

Wapiganaji wa zamani wa waasi nchini Cote d'Ivoire wakiondoka katika hoteli ya Golf, Abidjan, Desemba 16 mwaka 2010.
Wapiganaji wa zamani wa waasi nchini Cote d'Ivoire wakiondoka katika hoteli ya Golf, Abidjan, Desemba 16 mwaka 2010. Reuters

Mahakama ya kimataifa ya mjini The Hague ya ICC imetangaza kuchunguza waasi wa zamani waliomuunga mkono rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara kabla na baada ya uchaguzi mkuu uliopita nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Sanjari na hayo, Viongozi hao wa waasi wamefunguliwa mashtaka na mahakama ya nchi hiyo kwa uhalifu uliofanywa wakati wa mgogoro wa kisiasa mwaka 2010-2011 baada ya uchaguzi.

Hata hivyo, serikali ya Cote d'Ivoire inasema haitaingilia uhuru wa mahakama na kuwa huu ni utaratibu wa kawaida tu na watu wasubirie matokeo ya hayo yote.

Kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na kesi hiyo, Cherif Ousmane Fofana na Losseni, viongozi wawili wa waasi wa zamani walimuunga mkono Ouattara, ni miongoni mwa viogozi waliofunguliwa mashitaka. Viongozi hao waili walijihusisha na mambo mengi muhimu wakati wa vita dhidi ya majeshi ya Laurent Gbagbo.

Ni mara ya kwanza tangu 2011 watu ambao walimuunga mkono Ouattara kufuatiliwa na vyombo vya sheria. Kwa Jumla, zaidi ya watu ishirini wanakabiliwa na mashtaka haya mapya. Kambi ya rais wa zamani haijawekwa kando, jambo ambalo limeliridhisha Shirikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu.