Jumuia ya Afrika mashariki yamteua rais wa Uganda Yoweri Museveni kuwapatanisha wanasiasa Burundi, Sudan kusini yaadhimisha miaka minne ya uhuru

Sauti 21:36
Sayari ya dunia
Sayari ya dunia

Katika makala hii tunaangazia hatua ya viongozi wa jumuia ya afrika mashariki kumteua rais Yoweri Kaghuta Museveni wa Uganda kuwa mpatanishi mpya wa mzozo wa kisiasa unaolikumba taifa la Burundi na kuiomba serikali ikubali kuuahirisha uchaguzi mkuu hadi tarehe 30 julai, uchaguzi ambao ulikuwa umepangwa kufanyika mnamo tarehe 15 julai.Na huko nchini Sudan Kusini, wananchi waliadhimisha kumbukumbu ya miaka minne ya uhuru wa taifa hilo changa duniani lililojitenge na Sudan ya kaskazi namo mwaka 2011.Nchini Uganda wanasiasa wawili wenye umaarufu nchini humo, kukamatwa na polisi, wakati nchini DRC Uganda kupandisha bei ya Visa kwenye mipaka yake na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Kimataifa, tunazungumzia hatua ya ugiriki kuwasilisha mapendekezo mapya kwa wakopeshaji wa kimataifa, kuhusu namna ya kulipa deni lake.