MAURITIUS-SIASA-SHERIA

Mauritius: waziri ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela

Pravind Jugnauth mwaka 2011, katika mji mkuu, Port-Louis. Wakati huo alikua waziri wa fedha.
Pravind Jugnauth mwaka 2011, katika mji mkuu, Port-Louis. Wakati huo alikua waziri wa fedha. REUTERS/Ally Soobye

Uamuzi wa Mahakama unaweza kubadilisha mwelekeo wa matukio ya kisiasa nchini Mauritius. Waziri wa Teknolojia, Pravind Jugnauth, amehukumiwa kifungo cha miezi kumi na mbili kufuatia mgongano wa maslahi.

Matangazo ya kibiashara

Mtu huyu muhimu kwa serikali iliopo madarakani tangu Desemba mwaka 2014 amekamatwa kwa kesi ya zamani.

Katika kuhitimisha hatia dhidi ya Pravind Jugnauth, vyombo vya sheria vya Mauritius havijawatuhumu wafuasi pekee wa muungano wa vyama vilio madarakani kwa miezi saba sasa, lakini hata wafuasi wa vyama vingine vya upinzani vilihusishwa na tuhuma mbalimbali. Kwani waziri wa Teknolojia ni mtu muhimu kwa serikali. Hakika, Praving Jugnauth si mwingine ila mwana wa Waziri Mkuu Anerood Jugnauth. Ambaye, alikuwa akijiandaa kumrithi baba yake.

Lakini kwa kusubiri, vyombo vya sheria vimemkuta waziri huyo na hatia ya mgogoro wa maslahi baada ya kesi iliyodumu miaka mitano. Mwaka 2010, Praving Jugnauth, wakati huo akiwa waziri wa fedha, alitoa kibali kilichoruhusu kuondolewa kwa karibu dola milioni 5 kwa ajili ya kununua upya kliniki ambapo ndugu wa waziri huyo walikua na hisa. Upinzani ulibaini mambo mengi katika kesi hiyo, ukisema kuwa waziri alitoa kitita kikubwa kwa kununua kliniki hiyo ili kunufaisha familia yake.

Miaka mitano baadaye, majaji wawili wamesema Praving Jugnauth ana hatia kwa sababu alikuwa maslahi binafsi ya moja kwa moja katika shughuli hiyo. Praving Jugnauth alijiuzulu mara moja baada ya uamzi huo wa Mahakama wa kifungo cha miezi kumi na mbili jela, lakini amekata rufaa.